Monday, 18 January 2016

KASI YA RAIS MAGUFULI YAZIATHIRI HOTELI ZA KIFAHARI TANZANIA


Dr John Magufuli Rais wa Tanzania.

Hatua ya serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi kwa kuzuia wizara, taasisi na mashirika ya umma kukutana katika hoteli kwa shughuli mbalimbali za kikazi, imeanza kuleta athari  baadhi ya wamiliki wa hoteli wakisema wameathirika kimapato na sasa wako mbioni kupunguza wafanyakazi.

Kadhalika, baadhi ya wasomi wamesema licha ya dhamira nzuri ya serikali katika kuhakikisha inabana matumizi ili fedha zitakazopatikana zielekezwe katika miradi ya maendeleo, bado kuna haja ya kuangalia kwa umakini athari zake. Pia wameonya kuwa sekta ya hoteli ikiyumba itaathiri wajasiriamali wengi na sekta binafsi kwa ujumla.

Baada ya kuapishwa na kuingia madarakani Novemba 5, mwaka jana, Rais Dk. John Magufuli ilitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuipa nguvu ya kuwatumikia wananchi.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kupiga marufuku vikao vya kazi vya taasisi na mashirika ya umma kufanyika hotelini, kufanyika kwa hafla za kupongezana, kuadhimisha wiki mbalimbali zikiwamo za maji na Siku ya Ukimwi, warsha, semina, makongamano, mikutano na mafunzo.

Zingine ambazo sasa zinaelezwa kuathiri baadhi ya wajasiriamali na sekta binafsi ni pamoja na kufutwa kwa sherehe mbalimbali ikiwamo ya Uhuru, maadhimisho ya kitaifa na kimataifa yaliyokuwa yakiwalazimu wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi kutua Tanzania au kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

CHAMA CHA WENYE HOTELI
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), Latifa Sykes, alisema sekta ya hoteli ni moja ya maeneo yanayoajiri watu wengi kwa sababu ya kuangalia wageni na kushughulikia matukio mbalimbali, ikiwamo mikutano.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125