Friday, 22 January 2016

KUTOKA ADHABU YA KIFO HADI KUWA HURU BAHATI YA PEKEE.

Bendera ya Myanmar.


Rais wa Myanmar anayemaliza muda wake, Thein Sein, ameamuru kuachiwa huru kwa wafungwa 101 wakiwemo takribani 25 waliohukumiwa kwa makosa ya kisiasa.

Maafisa nchini humo wamesema msamaha huo unawahusu pia wafungwa 77 waliokuwa wamehukumiwa kifo na adhabu yao kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha.

Kwa mujibu wa chama cha wafungwa wa kisiasa nchini humo, miongoni mwa wafungwa 25 wa kisiasa, yumo raia wa New Zealand, Philip Blackwood, ambaye alihukumiwa mwezi Machi kwa kosa la kwenda kinyume na misingi ya kidini.

Wafungwa wengi wa kisiasa tayari wamekwishaachiwa huru kama sehemu ya mchakato wa mabadiliko chini ya utawala wa Rais Thein Sein tangu mwaka 2011.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125