Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kupiga kura katika mkutano wake wa kilele wa kila mwaka baadaye wiki hii kuhusu kuwapeleka wanajeshi 5,000 wa kulinda amani nchini Burundi, licha ya nchi hiyo kupinga vikali hatua hiyo.
Viongozi wa Umoja wa Afrika watakusanyika katika mji mkuu wa Addis Ababa siku ya Jumamosi na Jumapili ambapo kando na suala la Burundi, watamchagua mwenyekiti mpya wa AU kuchukua nafasi ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, wakati pia mikutano ya pembezoni ikitarajiwa kujumuisha mazungumzo yaliyokwama ya kumaliza vita na kufanikisha serikali ya umoja wa kitaifa nchini Sudan Kusini.
0 comments:
Post a Comment