Wednesday, 20 January 2016

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUIZURU BURUNDI LEO.


Chapa ya umoja wa mataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaanza ziara nchini Burundi leo Alhamis, katika juhudi za kutafuta amani wakati kukiwa na hofu kwamba nchi hiyo inaweza kutumbukia kwa mara nyingine katika ghasia za kikabila. 
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wana matumaini ya kumshawishi rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kukubali kupelekwa nchini mwake, wanajeshi 5000 wa Umoja wa Afrika watakaokuwa na jukumu la kuepusha vurugu. 
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power anayeongoza ujumbe huo unaozishirikisha pia Ufaransa na Angola, amesema ipo haja ya kuwepo kikosi cha kimataifa nchini Burundi kwa ajili ya kuwalinda raia. 
Wanadiplomasia lakini wamekiri kuwepo mgawanyiko kuhusu namna ya kuushughulikia mzozo wa Burundi, huku Balozi wa Angola Ismael Gaspar Martins akisema si lazima kuitaka Burundi kukubali kikosi cha Umoja wa Afrika, akisisitiza ni jukumu la nchi kuwalinda raia wake.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125