Thursday, 7 May 2015

WAINGEREZA WAPIGA KURA KWA MUSTAKABALI WA TAIFA LAO.

Waingireza wanapiga kura leo katika kinyang'anyiro kikali cha uchaguzi ambao huenda ukaamua hatima ya uanachama wa nchi yao katika Umoja wa Ulaya na kuongeza uwezekano wa kuwepo uhuru wa Scotland. 

Wapiga kura wanafanya uamuzi kati ya chama cha Kihafidhina cha siasa za wastani za mrengo wa kulia kinachoongozwa na Waziri Mkuu David Cameron na kile cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha Labour kinachoongozwa na Ed Miliband. 

Wakati viongozi wa vyama vyote viwili wakisisitiza kuwa wanaweza kupata moja kwa moja wingi wa kura katika bunge lenye viti 650, watahitajika bila shaka kushirikiana na vyama vidogo ili kuunda serikali. 

Uchunguzi wa maoni uliotolewa jana ulionyesha kuwepo kinyang'anyiro kikali baina ya vyama hivyo viwili vikuu. Takribani wapiga kura milioni 50 wamesajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125