Wednesday, 29 April 2015

NIGERIA INAFANYA UCHUNGUZI KWA WANAWAKE 293 WALIOKOMBOLEWA KUTOKA KWA BOKO HARAMU.


Baada ya kufanya uokoaji mkubwa wa wasichana wadogo 200 na wanawake 93 kutoka katika msitu ambao ni ngome kuu ya wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram, jeshi la Nigeria linawaondoa wanawake hao na linapanga uchunguzi wa afya zao na hali zao kiakili.

Kanali Sani Usman amesema wengi wako katika hali ya kiwewe na fadhaa. Jeshi amesema linapeleka wataalamu wa afya na uchunguzi wa afya ya akili kuwachunguza wanawake hao.

Ameongeza kuwa bado haijafahamika iwapo baadhi yao ni miongoni mwao wasichana 219 ambao bado hawajulikani waliko zaidi ya mwaka mmoja baada ya kutekwa nyara kutoka katika shule mjini Chibok, mji ulioko kaskazini mashariki , katika utekaji nyara mkubwa ambao umezusha hasira duniani.

Kuondolewa wanawake hao kutoka msitu wa Sambesi ulianza jana lakini Usman hakusema wanawake hao wamepelekwa wapi.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125