Wednesday, 29 April 2015

MUGABE ASEMA AFRICA INA RASILIMALI NYINGI NA UMASIKINI WA KUTOSHA.


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema leo kwamba licha ya utajiri wa mali asili ulioko katika nchi za kusini mwa Afrika lakini kiasi ya asilimia 70 ya wananchi wa nchi hizo , wanaishi katika umasikini mkubwa , na kuwataka viongozi wa eneo hilo kuanzisha viwanda badala ya kusafirisha nje mali ghafi zinazopatikana katika nchi hizo.

Mugabe amesema hayo katika hotuba ya ufunguzi katika mkutano wa kilele wa kimkoa wa jumuiya ya maendeleo ya uchumi kusini mwa Afrika SADC katika mkutano wao leo.

Mashambulizi dhidi ya wahamiaji wanaoishi nchini Afrika kusini hata hivyo yanatishia kugubika mkutano huo wa kilele nchini Zimbabwe wakati viongozi wakikusanyika kuhimiza ukuaji wa viwanda.

Lakini amelikwepa suala hilo katika hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano huo wa SADC ambapo Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini anahudhuria .

Rais Mugabe ameeleza mshituko na kuchukizwa kwake na ghasia za chuki dhidi ya wageni mjini Johannesburg na Durban ambako kiasi watu saba wameuwawa.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125