Sunday, 26 April 2015

IDADI YA WALIOKUFA KWA TETEMEKO LA ARDHI NEPAL YAFIKIA 5000


Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kutafuta miili ya wahanga wa tetemeko baya kabisa la ardhi nchini Nepal, huku idadi rasmi ya wahanga wa tetemeko hilo ikizidi 2,500. 

Waziri wa mambo ya ndani wa Nepal amethibitisha idadi ya vifo kutokana na tetemeko la jana lenye ukubwa wa 7.9 kipimo cha richter kuwa 2,500, huku idadi kubwa zaidi ya wahanga ikiripotiwa katika mji mkuu Kathmandu. 

Watu wengine 50 wameuawa katika nchi jirani ya India, waakati waathirika wengine wameripotiwa nchini China na Bangladesh. Zilzala hilo lilifika hadi kwenye mlima Everest, ambako watu 18 wameripotiwa kuuawa na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia maporoko makubwa ya theluji yaliyosababisha na tetemeko hilo. Polisi imeripoti kuwa watu zaidi ya 5000 wamejeruhiwa.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125