Picha hii inamuonyesha waziri mkuu wa Tanzania na wananchi wa hali ya chini. |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali imeandaa sera, taratibu na sheria madhubuti zitakazosimamia uvunaji wa gesi nchini.
Pinda amesema jijini Dar es Salaama katika mkutano 20 ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Umaskini (Repoa) uliokuwa unajadili namna gani nchi inaweza kufaidika na matumizi ya gesi.
Waziri Mkuu amesema katika sala la gesi serikali imejipanga ili kuepuka kuingiza Watanzania katika machafuko.
Pinda amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) litahakikisha panakuwapo kampuni za uvunaji gesi zenye ubora.
Mbunge wa Moshi Vijijini, Dk. Cyril Chami, aliitaka serikali ya Tanzania kujisimamia yenyewe katika swala zima la gesi huku wageni wawe wanatoa utalaamu na ushauri tu ili kumwezesha Mtanzania wa kipato cha chini kufaidika na bidhaa hiyo.
Ameongeza: wanasiasa wakae karibu na wataalamu ili kuwa na uwelewa wa bidhaa ya hiyo, kuepuka kufanya maamuzi muhimu mbungeni kisiasa na kuwaumiza Watanzania wengi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Prof. Samuel Wangwe, alisema Taasisi hiyo ipo tayari kuisaidia serikali kuhakikisha mambo yanayohitaji utafiti na utalamu wa gesi yanafanyika ili kuhakikisha uchumi wa Watanzania unakua.
0 comments:
Post a Comment