Hii ni moja ya ndege za kivita. |
Ndege za kijeshi za Jordan zinashiriki katika operesheni inayoongozwa na Saudi Arabia pamoja na washirika wake mataifa ya Kiarabu dhidi ya wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen.
Taarifa ya pamoja ya mataifa matano ya ghuba imesema Saudi Arabia , Umoja wa falme za Kiarabu , Kuwait, Bahrain na Qatar zimeamua kuchukua hatua kuilinda Yemen dhidi ya kile ilichokiita uvamizi wa wanamgambo wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani Adel-al-Jubeir amesema lengo ni kuilinda serikali halali ya Yemen.
Jordan ina mahusiano ya karibu na mataifa ya Ghuba na inaitegemea Saudi Arabia kwa kiasi kikubwa kuusaidia uchumi wake.
Wakati huo huo wizara ya mambo ya kigeni ya China imesema leo kwamba inawasi wasi mkubwa juu ya hali inayoendelea kuharibika nchini Yemen, baada ya Saudi Arabia kutangaza kuwa imeanzisha operesheni za kijeshi nchini humo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Hua Chunying amewaambia waandishi habari kwamba China inazitaka pande zote kuchukua hatua kwa mujibu wa maazimio ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen na kutatua mzozo huo kwa njia ya mazungumzo.

0 comments:
Post a Comment