Saturday, 28 March 2015

BOKO HARAM WATIA DOA UCHAGUZI MKUU NIGERIA WAFANYA MAUAJI KWENYE MSURURU WA KURA.


Kundi la kigaidi la Boko Haram leo hii limeuwa watu sita katika mashambulio mawili tofauti yaliyofanywa katika Jimbo la Gombe na Yobe kwenye vituo vya kupiga kura kaskazini-mashariki mwa Nigeria. 
 
Mikasa hiyo inatokea wakati mamilioni ya watu wakiwa katika misururu ya kutimiza wajibu wao wa msingi wa kidemokrasia wa kuchagua rais wa taifa hilo katika maeneo tofauti.
 
 Umar Hammaga aliyeshuhudia mkasa wa kwanza alisema wanamgambo walifyatua risasi hewani na kuwaonya wakaazi wasishiriki katika uchaguzi huo venginevyo wangeliwauwa wote.Umar ni mkazi wa kijiji kimoja katika jimbo la Gombe. 
 
Hata hivyo aliongeza kusema kuwa polisi walifanikiwa kurejesha hali ya utulivu katika eneo hilo na wapiga kura walirejea katika vituo vya kupiga kura. Mkuu wa Polisi katika jimbo la Yobe Danlad Marcus alisema katika kila tukio katika maeneo hayo waliwawa watu watatu, watatu.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125