Thursday, 26 May 2016

JINAMIZI LA KUZAMA BAHARINI BADO LINAWAANGAMIZA WATU MEDITERANIAN.

0 comments


Mamlaka nchini Italia zinasema boti moja ya wahamiaji imezama kwenye Bahari ya Mediterenia hivi leo, siku mbili tu baada ya mkasa mwengine kama huo. Msemaji wa jeshi la walinzi wa pwani ya Italia anasema hadi sasa watu 88 wameokolewa, huku idadi kamili ya waliopoteza maisha ikiwa haijajulikana. Meli za uokozi za Umoja wa Ulaya zimethibitisha kuopoa maiti 20 hadi sasa. 
Hata hivyo, shirika la habari la Ansa limesema kiasi cha watu 30 wamefariki dunia kutokana na ajali ya leo. Katika boti iliyozama hapo jana, watu watano walithibitika kufa maji. Idadi ya boti za wahamiaji imepanda sana wiki hii, kutokana na kuanza kwa majira ya kiangazi na pepo za matilai. Jumla ya operesheni 20 za uokozi zinaendelea. 
Hadi juzi, Jumanne, idadi ya wahamiaji waliokwishawasili kwenye fukwe za Italia ilikuwa imeshuka kwa asilimia 9, lakini bado serikali inahaha kupata mahala pa kuwaweka wahamiaji zaidi ya 115,000 ambao tayari wamo nchini humo.
SOMA ZAIDI ...

Monday, 21 March 2016

RAIS MAGUFULI ATII AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAMU APELEKA BASTOLA POLISI KUHAKIKI NINI MAONI YAKO.?

0 comments


Rais wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli akitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda la kuhakikisha kila anaemiliki silaha anafika Polisi ili kuhakiki juu ya umiliki wake.
SOMA ZAIDI ...

DR SHAIN ASHINDA KWA KISHINDO ZANZIBAR, NI USHINDI WA 91%

0 comments



Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha amemtangaza Dr. Mohammed Shein kuwa Rais wa Zanzibar kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016 kwa asilimia 91.4.
 
Kwa mujibu wa Jecha, Shein amepata ushindi wa kishindo wa kura 299,982 ambazo ni sawa na asilimia 91.4. Nafasi ya pili imeshikiliwa na mgombea urais wa ADC, Hamad Rashid aliyepata kura 6,734 huku Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 6,076.

Kutokana na matokeo hayo, Dk. Ali Mohamed Shein ndiye atakayeendelea kuiongoza Zanzibar kwa muhula wake wa mwisho kwa mujibu wa Katiba.
SOMA ZAIDI ...

TAZAMA MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI ZANZIBAR.KWA MAJIMBO 5

0 comments
Matokeo ya Urais: Wilaya ya Chake katika Majimbo ya OLE, ZIWANI, CHONGA, WAWI na CHAKE

1458536627875.jpg 
1458536659331.jpg 
1458536668390.jpg 
1458536677820.jpg 
1458536689280.jpg 
1458536717313.jpg
SOMA ZAIDI ...

MSHUKIWA MKUU WA MAUAJI YA RWANDA AREJESHWA RWANDA KUTOKA CONGO.

0 comments


Waziri wa sheria wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Alexis Thambwe Mwamba ametangaza kuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya halaiki ya Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994, Ladislas Ntaganzwa amerejeshwa nchini Rwanda kukabiliwa na mashitaka. Kukamatwa kwa Ntaganzwa mwaka jana nchini Congo kulikuja zaidi ya miongo miwili tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa nchini Rwanda. Mshukiwa huyo aliyekuwa akisakwa sana alisafirishwa jana kutoka Kinshasa hadi Kigali, miezi mitatu baada ya kukamatwa. Maafisa wa Rwanda wamesema watamfungulia mashitaka tisa ya mauaji ya halaiki meya huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 53. Ntaganzwa pia atashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kukiuka makubaliano ya Geneva kwa kuhusika katika kupanga na kuagiza mauaji makubwa ya zaidi ya Watutsi 20,000 katika kipindi cha siku nne.
SOMA ZAIDI ...

MAUAJI YA KUTISHA HUKO KYELA MBEYA TANZANIA

0 comments


Watu watatu wamefariki dunia kwa kunyongwa na miili yao kuchomwa moto ndani ya nyumba ya wageni iliyopo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Mauaji hayo yamegubikwa na utata kutokana na mazingira ya tukio hilo kuwahusisha wapangaji wa nyumba hiyo usiku wa kuamkia jana.

Mmiliki wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Kyela Kati, Boniface Mtengela alisema waliouawa ni watatu kati ya watu wanne waliofika kwa pamoja saa nne usiku jana.

Alisema watu hao walikuwa wanaume watatu na mwanamke mmoja na waliouawa ni mwanamke na wanaume wawili.

Mtengela alisema wanaume wawili walijiandikisha kwa jina la Ali Hassan na mwanamke la Mariam.

“Mwanamume mmoja alipanga chumba namba 14, mwingine 105 na mwenye mke alipanga chumba namba 15. 

"Waliokutwa wamekufa ni wanaume wawili wa vyumba na 14 na 105 pamoja na mwanamke huku mwanamume mwenye mke akitoroka,” alisema.

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kyela, Francis Mhagama alisema uchunguzi wa miili ya marehemu hao umebaini kuwa waliuawa kwa kunyongwa kisha kuchomwa moto baada ya kumwagiwa mafuta ya taa.

Uchunguzi katika eneo la tukio ulibaini miili yao iliungua, lakini chumba na magodoro havikuungua. Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kyela Kati, Timoth Luvanda alisema usiku wa tukio hilo hakusikika kelele zozote.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi hakupatikana kuzungumzia tukio hilo wala kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba hiyo na kuhojiwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela.

Mhudumu wa nyumba hiyo, Hagai Yohana alisema mgeni mmojawapo aliondoka kabla ya saa 12 alfajiri akiwa na kidumu na mfuko wa rambo.

Alisema wageni wote waliandikisha kuwa ni wafanyabiashara na hawakuwa na mizigo. 

Picha na habari ni kwa mujibu wa mtandao wa HARUBUTZ
SOMA ZAIDI ...

Tuesday, 15 March 2016

KOREA YA KASKAZINI ANAENDELEA KUITAMBIA DUNIA.

0 comments

kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un , amesema yakwamba nchi yake itafanya majaribio ya kurusha silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu katika muda mfupi, shirika rasmi la habari KCNA hili toa taarifa Jumanne.
SOMA ZAIDI ...
 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125