Waziri wa sheria wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Alexis Thambwe Mwamba ametangaza kuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya halaiki ya Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994, Ladislas Ntaganzwa amerejeshwa nchini Rwanda kukabiliwa na mashitaka. Kukamatwa kwa Ntaganzwa mwaka jana nchini Congo kulikuja zaidi ya miongo miwili tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa nchini Rwanda. Mshukiwa huyo aliyekuwa akisakwa sana alisafirishwa jana kutoka Kinshasa hadi Kigali, miezi mitatu baada ya kukamatwa. Maafisa wa Rwanda wamesema watamfungulia mashitaka tisa ya mauaji ya halaiki meya huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 53. Ntaganzwa pia atashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kukiuka makubaliano ya Geneva kwa kuhusika katika kupanga na kuagiza mauaji makubwa ya zaidi ya Watutsi 20,000 katika kipindi cha siku nne.
Browse » Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment