FC Barcelona jana walifaulu kuwanyuka Celta Vigo mabao 6-1 na kubakia kileleni mwa ligi kuu ya Hispania na pointi 57 mbele ya Atletico Madrid ambao wana pointi 54 huku wapinzani wao wa jadi Real Madrid wakifuata katika nafasi ya tatu na pointi 53.
Mabao ya Barca yalifungwa na Lionel Messi katika kipindi cha kwanza huku Luis Suarez alikunga hat-trick katika dakika za 59, 75 na 81. Mabao mengine yalifungwa na Ivan Rakitic pamoja na Neymar Neymar da Silva Santos JĂșnior huku John Guidetti akifungia Celtic Vigo bao la kipekee kwa njia ya penalti.
0 comments:
Post a Comment