waziri wa mambo ya ndani Thomas de Maizière amesema wakimbizi wanaishitaki serikali kutokana na kusubiri kwa muda mrefu kupata jawabu la maombi yao ya kutafuta hifadhi. Hili linakuja baada ya mamia kwa maelfu ya kesi kuwa hazikufanyiwa kazi kwa miezi kadhaa sasa. Hata hivyo,
ofisi ya shirikisho inayowawakilisha wahamiaji imesema kesi hizo zinahusu wahamiaji waliowasili mwaka 2014, na sio mwaka 2015 ambapo zaidi ya wahamiaji milioni moja waliwasili nchini.
Waziri huyo alikabiliana na malalamiko hayo kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi wa kushughulikia maombi ya wahamiaji kwa asilimia 40. Zaidi ya wakimbizi 440,000 wameomba hifadhi nchini Ujerumani tangu mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment