Thursday, 21 January 2016

NCHI ZA MAGHARIBI ZAAPA KULIANGAMIZA KUNDI LA IS.



Mawaziri wa ulinzi wa nchi za magharibi wanaokutana jijini Paris wamekubaliana kuongezea nguvu zaidi kampeni dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Iraq na Syria.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza, Michael Fallon, amesema kampeni hiyo ya pamoja italenga zaidi uongozi wa IS na miundombinu(mawasiliano na njia zao za usafirishaji).

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Ash Carter amesema wana nia kuu tatu ambazo ni kuisambaratisha IS katika ngome zake za Raqqa na Mosul, kupambana na matawi yake duniani kote na kulinda raia.

Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 27 zikiwemo Iraq na nchi kadhaa za kiarabu watakutana mjini Brussels mwezi ujao.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125