Picha za satelaiti zimeonesha makaburi matano yaliyozikwa watu wengi kwa pamoja nje kidogo na mji mkuu wa Burundi Bujumbura, katika eneo ambalo watu walioshuhudia walisema kwamba vikosi vya usalama vilifanya mauaji kadhaa mwezi Desemba, haya ni kwa mujibu wa shirika la Amnesty International.
Hata hivyo msemaji mkuu wa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza, hakupatikana kutoa tamko la upande wa serikali juu za ripoti hizo za Amnesty International.
Mataifa ya Afrika yatajaribu kumshinikiza rais Nkurunziza kukubali kupokea askari wa kulinda amani nchini humo, katika mkutano wa kilele utakaofanyika wiki hii ili, kuizuia Burundi isitumbukie tena katika vita vya kikabila lakini hakuna matumaini kwamba rais huyo atakubaliana nao.
0 comments:
Post a Comment