Thursday, 28 January 2016

HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYESHINDIKANA DUNIANI.





Nyota wa tenisi nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams anatarajiwa kuandikisha rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushinda michuano mingi zaidi duniani endapo atashinda fainali ya wanawake ya mchuano wa Australian Grand Slam siku ya jumamosi.

Serena alijipatia nafasi hiyo mwafaka baada ya kumbwaga Agnieszka Radwanska katika seti mbili 6-0, 6-4 wakati wa mchuano wa nusu fainali .

Iwapo nyota huyo atambwaga Angelique Kerber, siku ya Jumamosi basi atakuwa ameshinda taji 22.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125