Basi likivutwa. |
Takriban watu 10 waliaga dunia na wengine 21 kujeruhiwa jana usiku (Jumatatu) baada ya basi la abiria kuanguka ndani ya bonde katika jimbo la Meghalaya, kaskazini mashariki mwa India, taarifa ya polisi imesema.
Basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Guwahati kuelekea Hailakandi lilipopata ajali hiyo katika wilaya ya East Jaintia Hills District. Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment