Rais Museven wa Uganda |
Mwendeshamashitaka wa ngazi ya juu nchini Uganda Joan Kagezi ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Kampala. Polisi nchini humo imesema huenda kuuawa kwake kuna uhusiano na kesi aliyoiendesha dhidi ya washukiwa wa mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyouwa watu 79 mjini Kampala mwaka 2010, ambayo kundi la al-Shabab la nchini Somalia lilikiri kuhusika.
Bi Kagezi alipigwa risasi saa mbili usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Kiwatule, umbali wa km 13 kutoka katikati mwa jiji la Kampala, aliposimamisha gari lake.
Msemaji wa polisi ya Uganda Patrick Onyango amesema wanaume wawili walikuwa wakimfuata kutumia pikipiki aina ya bodaboda, na kwamba alikata roho muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini. Wiki iliyopita ubalozi wa Marekani ulikuwa umetahadharisha juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi katika mji huo.
0 comments:
Post a Comment