Monday, 23 March 2015

WHO YALAUMIWA KWA KUSHINDWA KUDHIBITI EBOLA MAPEMA LICHA YA KUWA NA UWEZO WA KUFANYA HIVYO.



Mwili wa mtu aliyekufa kwa Ebola ukihudumiwa na daktari kabla ya maziko huko LIBERIA. 


shirika la madaktari wasio na mipaka limeitupia lawama shirika la WHO kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kushughulikia suala la Ebola.

Shirika la madaktari wasio na mipaka limetoa ripoti kuhusu hatua zilizochukuliwa na dunia dhidi ya ugonjwa huo , ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 10,000 na wengine 25,000 wameambukizwa tangu kugundulika kwa ugonjwa huo Machi mwaka 2014, wengi wao nchini Guinea , Liberia na Sierra Leone.

Shirika la kutoa misaada ya kiafya la MSF limesema miezi imepotea na maisha yamepotea kwasababu ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa , ambalo linawajibu wa kuratibu masuala kama hayo ya dharura , na ambalo lilikuwa na uwezo wa kuudhibiti ugonjwa wa Ebola , lilishindwa kuchukua hatua za haraka ama zakutosha.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125